Kukumbatiana ni njia nzuri sana ya kumaliza migogoro katika mahusiano

 


Kuna siku fulani nilipata wasaa mzuri wa kusoma kitabu fulani hivi cha saikolojia, katika kitabu hicho yapo mambo mengi sana ambayo yameandikwa hususani tabia za mwanadamu kiujumla. Moja kati ya vitu ambavyo vilinishangaza ni pamoja ya kwamba mgusano wa mtu mmoja na mwingine ni dawa tosha kwa watu wenye tofauti.


Nilipokuwa nikiendela kusoma kitabu hicho nikaleta fikra zangu katika maisha ya kawaida nikaja nikagundua ya kwamba watu wengi wakikosana katika jamii zetu watu ambao wakitokea kwa lengo la kuwapatanisha basi huwa uwamuliwa watu hao wapeane mikono ikiwa ni ishara ya wazi kwamba kila mmoja moyo wake ni safi na hauna kinyongo na mtu  mwingine.


Nikaendelea kusoma kitabu hicho ambapo tena nikakutana na faida kadha wa kadha la kumbatio katika mahusiano hasa pale inapotokea watu fulani wamekwazana katika mahusiano ya kimapenzi.


 Ambapo nilikuja kugunundua ya kwamba kukumbatiana katika mahusiano ya kimapenzi inaweza kuwa ni njia nzuri sana ya kumaliza tofauti za wapendanao katika mahusiano, hii ni kwasababu watu waligombana pindi wanapokumbatiana basi huzalisha joto na hisia za Upendo ambapo kila mmoja wao hujikuta anamsemehe yule ambaye amemkosea.


Kitu kingine  ambacho nimekigundua katika kukumbatiana,  kumkumbatia mwenza wako wakati mnapokuwa katika malumbano ya hoja yenu taratibu  inabadilisha hali  yote ya machafuko.


 ukimkumbatia mwenza wako wakati wa malumbano huwa inaleta hali tofauti, haiwezi kuwa kama siku zote ambazo umezoea, imegundulika kuwa inakuwa na hisia za kweli, mtu anaweza kujisikia vizuri zaidi kuliko ile kawaida ya siku zote, inaondoa  hali ya kuwa na shaka lolote.


Mpaka kufikia hapo sina la ziada nakutakia utumiaji mwema wa njia hii ya kumbatio hasa pale unapokuwa umegombana na mwenza wako.


Na. Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad