Kuna udhaifu kwenye kupambana na nzige” Mkenda




Serikali imesema hairidhishwi na utendaji wa shirika la kukabiliana na nzige wa jangwani la Afrika Mashariki lenye makao yake makuu nchini Ethiopia, kutokana na udhaifu katika kupambana na nzige hao ambao wameendelea kuathiri nchi wanachama wanaohudumiwa na shirika hilo.
Aidha serikali imeelezea kusikitishwa kwake na hatua ya Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Dk. Nzoka pamoja na kupewa taarifa kwamba Waziri wa Kilimo wa Tanzania, Prof Adolf Mkenda anamtafuta lakini bado hajaoneshwa kujali taarifa hiyo.

Waziri Mkenda amesema kutokana na udhaifu huo, serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imewasiliana na Balozi wa Tanania nchini Ethiopia na kumuelekeza amtafute Mkuu wa Shirika hilo kujua tatizo liko wapi.

“Haiingii akilini kwamba tunaomba msaada katika shirika la nzige wekundu wakati, shirika la kupambana na nzige wa jangwani halitekelezi wajibu wake….tumechukua Helkopta na ndege ya kukabiliana na nzige wekundu, huku hii ya kwetu imepaki hapa uwanja mdogo Moshi na haina rubani,” Mkenda

Amesema ndege ya kukabiliana na nzige wa jagwani ipo katika uwanja wa Moshi huku rubani wake akipelekwa Kenya jambo ambalo linatia shaka kuhusu utendaji wa shirika hilo hususan kipindi hiki ambacho nchi wanachama limevamiwa na nzige wa jangwani.

“Kama utendaji wa shirika hili uko hivi, haishangazi kuona nzige hawa wanaendelea kuathiri nchi wanachama na hakuna jitihada za makusudi kuwakabili…ikumbukwe Tanzania ni moja ya nchi mbili ambazo zinalipa vizuri ada zake za uanachama wa shirika hilo,” Mkenda

Aidha Waziri Mkenda amesema mapambano dhidi ya wadudu hao yanaendelea vyema kwa kushirikiana serikali ya Kenya kutokana na ukweli kwamba nzige hao wanauwezo wa kutembea Km 80 kwa siku hivyo ni rahisi kutoka eneo moja hadi jingine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad