Luis Aweka Rekodi Tatu CAF



AKITARAJIA kujitupa uwanjani kesho, kiungo mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone, ameweka rekodi tatu katika dakika 90 alizocheza katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Rekodi hizo alizoziweka kiungo huyo ni katika mchezo uliopita dhidi ya Al Ahly ya nchini Misri uliopigwa wiki moja iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.


Staa huyo kesho anatarajiwa kuiongoza timu yake ya Simba katika mchezo wa tatu wa michuano hiyo mikubwa itakapovaana na Al Merrikh ya Sudan.

Nyota huyo reodi ya kwanza aliyoiweka ni ya kushinda tuzo ya bao bora la wiki alilolifunga katika mchezo dhidi ya Al Ahly kwa shuti kali nje ya 18.


Rekodi ya pili aliyoiweka ni ya kuingia kwenye kikosi bora cha wiki cha michuano hiyo mikubwa Afrika akiwa pamoja na beki wa kati wa timu hiyo, Joash Onyango.


Nyingine ni tuzo ya mchezaji bora wa wiki aliyechaguliwa juzi Jumanne baada ya Caf kumpendekeza kutokana na kiwango kikubwa alichokionyesha kwenye mchezo wa Ahly.


STORI NA WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad