Mahakama ya Malyasia imebadilisha sera inayopiga marufuku watu wa dini ya Kikristo kutumia jina ‘Allah’ kumaanisha Mungu, ikiwa ni hatua ya hivi karibuni katika miongo kadhaa iliokumbwa na mzozo wa kisheria kuhusu jina hilo.
Suala la wasio Waislamu kutumia neno Allah awali limekuwa likizuwa hali ya wasiwasi na vurugu nchini Malaysia.
Waislamu ni thuluthi mbili ya idadi ya watu lakini kuna jamii kubwa za Kikristo.
Jamii hizo za Kikristo zinahoji kwamba zinatumia jina Allah, kumaanisha Mungu kwa karne kadhaa na kwamba uamuzi huo unakiuka haki yao.
Katiba ya Malaysia inawahakikishia raia wake uhuru wa dini. Lakini hofu ya kidini imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.
‘Ni haramu na ukiukaji wa katiba’
Mwaka 2008 , utawala wa Malaysia ulikamata kaseti za Lugha ya Malay kutoka kwa Jill Ireland Lawrence Bill , Mkristo , katika uwanja wa ndege baada ya kubaini kwamba nakala zilizorekodiwa zilikuwa zikitumia jina Allah.
Bi Bill baadaye alienda mahakamani akipinga marufuku ya Wkristo kutumia neon Allah katika machapisho yao.
Siku ya Jumatano – baada ya muongo mmoja mahakama iliamuru kwamba alikuwa na haki kutoadhibiwa kulingana na dini yake.
Katika uamuzi wake , jaji Nor Bee aliamuru kwamba neno Allah – pamoja na maneneo mengine matatu kutoka kwa lugha ya Kiarabu ”Kaabah”, Baitullah { Nyumba ya Mungu} na ”Solat”{ Ibada} yanaweza kutumika na Wakristo.
Hakimu Nor Bee alisema kuwa agizo lililopiga marufuku utumiaji wa maneno manne lilikuwa “kinyume na sheria na katiba pia”.
“Uhuru wa kutambua na kuendeleza matendo ya dini yanastahili kujumuisha haki ya kuwa na nyenzo ya dini yenyewe,” alisema.
Hii sio mara ya kwanza mahakama ya Malaysian imegawanyika juu ya matumizi ya neno “Allah”.
Katika kesi tofauti, gazeti la mahakama ya Kikatoliki – The Herald – ilishitaki serikali baada ya kusema kuwa haiwezi kutumia maneno ya lugha ya Malay kuelezea Mungu wa Kikiristo.
Mnamo mwaka 2009, mahakama moja ilitoa uamuzi uliopendelea gazeti la The Herald na kuwaruhusu kutumia neno hilo katika uamuzi uliochochea chuki ya kidini kati ya Waislamu na Wakiristo.
Makumi ya makanisa kadhaa na kumbi za kusali kwa waumini wa dini ya Kiislamu yalivamiwa na kuchomwa moto.
Mwaka 2013, uamuzi huo ulibadilishwa na mahakama ya rufaa ambayo ilirejesha marufuku hiyo.
Alhamisi, Malaysia Muafakat Nasional – muungano wa kisiasa- ulisema kuwa uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama ya juu kupelekwa katika mahakama ya rufaa, kulingana na chombo cha habari cha eneo cha The Star.