Marais zaidi ya 10 wanatarajiwa kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa heshima zao za mwisho kesho katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa ‘twitter’ Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa orodha ya marais hao aitaitoa saa nane mchana katika kikao chake na wanahabari.
“Marais zaidi ya 10 kumuaga Dkt. John Pombe Magufuli Uwanja wa Jamhuri kesho Dodoma. Orodha na taarifa kamili itatolewa leo saa nane kamili mchana katika mkutano na waandishi wa habari,” ameandika Msemaji wa Serikali.
Zoezi la kutoa heshima za mwisho linaendeleo leo katika viwanja vya Uhuru Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya pili na kesho wananchi na wa Jiji la Dodoma pamoja na viongozi kutoka mataifa mbalimbali wataaga na baadaye mwili utaelekea Zanzibar kabla ya kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa.