Waziri Mpya wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken amekutana na maafisa wa ngazi ya juu kabisa wa China usiku wa Alhamis, mkutano uliokuwa na lengo la kujenga msingi wa ushirikiano wa kuaminiana kwa pande zote mbili.
Tough talk at first face-to-face US, China meeting in Biden era
Kabla ya mkutano huo mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China Yang Jiechi na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi na Msemaji wa Joe Biden walisema lengo ni kuibua masuala yenye kusababisha wasiwasi na vilevile kuyatafutia ufumbuzi.
Blinken na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani, Jake Sullivan wanatarajiwa kuwasilisha mada za masuala tata likiwemo la namna China inavyoshughulika na jamii ya wachache wa Waislamu wa Uighur, ambao wapo katika jimbo la Xinjiang, suala la Hong Kong, pamoja na hali ya kibiashara isiyo ya haki ya taifa hilo.
China kwa upande wake inasema itapigania kuondoshwa kwa tozo la ushuru uliowekwa na utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.