Polisi wa Texas nchini Marekani, waliruhusu wahamiaji haramu ambao walikwenda mpakani kuomba hifadhi kuingia nchini, licha ya vipimo vyao kuonyesha kuwa na maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19).
Katika taarifa iliyotelwa kwenye tovuti ya kituo cha Fox News, iliarifiwa kwamba polisi wa kushika doria mpakani Texas waliwaachilia zaidi ya wahamiaji haramu 100 ambao wameingia Mexico kupata hifadhi tangu mwisho wa Januari, licha ya matokeo ya vipimo vyao kuonyesha wana Covid-19, na kuwaruhusu kusafiri kwa hiari yao.
Msemaji wa mamlaka ya mpaka wa mji wa Brownsville, Felipe Romero, alisema kuwa asilimia 6.3 ya wahamiaji ambao wamekwenda tangu Januari 25 wamekutwa na Covid-19 na kwamba wahamiaji 108 waliruhusiwa kusafiri ndani ya nchi kama inavyotakiwa na sheria, ingawa hali yao ya afya inajulikana.
Akibainisha kuwa "hawana mamlaka ya kumzuia mtu ambaye ana Covid-19 kusafiri ndani ya Marekani" , Romero aliongezea kusema kuwa waliwashauri watu hawa kujitenga na kufuata miongozo ya Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa ( CDC).
Wahamiaji haramu wanaokwenda Marekani, kikawaida huachiliwa huru baada ya ukaguzi wa lango la forodha kukamilika, na kuvishwa kifaa cha ufuatiliaji kwenye kifundo cha mguu. Wahamiaji hao huhitaji kuanzisha taratibu rasmi za makazi baada ya kufikia sehemu za Marekani wanazotaka kukaa.