Mbappe aivusha PSG robo fainali ligi ya mabingwa



Mshambuliaji nyota wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, Kylian Mbappe amefanikiwa kuisaidia klabu yake kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kufunga bao moja katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao moja dhidi ya Barcelona usiku wa jana.



Baadhi ya matukio ya kwenye mchezo wa usiku wa jana PSG 1-1 Barcelona.


Mbappe alifunga bao hilo dakika ya 31 kwa mkwaju wa penalti kabla ya Lionel Messi kuisawazishia Barcelona dakika ya 37 kwa mkwaju wa penalti. Bao hilo ni la nne kwa Mbappe katika michezo miwili dhidi ya Barcelona baada ya kuwafunga mabao 3 kwenye ushindi wa 4-1 kwenye mchezo wa kwanza.


Nyota huyo wa PSG, ameifanya klabu yake hiyo ifuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 5-2 na kuweka rekodi ya kuwatoa miamba hiyo ya soka ya nchini Hispania kwa mara ya kwanza katika awamu 4 za nyuma walizokutana ikiwemo Barcelona kupindua kipigo cha 4-0 na Barca kushindi 6-1 mwaka 2017.


PSG ambao ni makamu bingwa wa michuano hiyo, wamechagiza kuandika rekodi ya michezo ya robo fainali itakayo cheza mwezi ujao kuchezwa kwa mara ya kwanza bila timu ya Lionel Messi au Cristiano Ronaldo kuwepo tokea msimu wa mwaka 2004-2005.


Kwa upande wa Mbappe aliyoonesha kiwango bora na kuwa gumzo duniani kwasasa, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufikisha mabao 25 akiwa na umri wa miaka 22 na siku 80 na kumpiku Messi aliyefunga mabao hayo akiwa na miaka 22 na siku 286.


Sasa mbappe amefkisha jumla ya mabao 6 kwenye michuano hiyo, mabao 4 nyuma ya kinara wa upajichaki mabao Braut Erling Haaland wa Borrusia Dortmund mwenye mabao 10.


Baada ya kufuzu hatua hiyo, droo ya kupanga nani na nani kuumana robo fainali na nusu fainali kujulikana siku ya kesho, Ijuma ya tarehe 12 mwezi huu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad