Mfahamu Anna Mwakasege, Rubani Aliyesafirisha Mwili wa JPM Dodoma




Baada ya kukamilika kwa shughuli za kumuaga Hayati Dk. John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam, mwili wake ulisafirishwa kwa ndege kwenda jijini Dodoma!

 

 

Kama ulifuatilia kwa makini tukio hilo, utagundua kwamba ndani ya ndege hiyo, Airbus A220 kulikuwa na marubani wawili na mmoja kati yao, ni mwanamke! Ndiyo! Mwanamke, tena wa Kitanzania! Mnyakyusa kutoka mkoani Mbeya!

 

 

Huyu si mwingine bali ni Anna Tusajigwe Mwakasege! Rubani mwanamke ambaye anaingia kwenye historia ya kuusafirisha mwili wa hayati Magufuli kwa ndege, si kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma pekee bali pia kutoka Dodoma kwenda Zanzibar na baadaye kutoka Zanzibar kuelekea Mwanza na hatimaye Chato.

 

 

Pengine sasa una shauku kubwa ya kutaka kujua mwanamke huyu ni nani? Imekuwaje akaingia kwenye historia kubwa ya kuusafirisha mwili wa kipenzi cha Watanzania, Dk. John Pombe Magufuli aliyefariki Machi 17, 2021 jijini Dar es Salaam?

 

 

Anna Mwakasege, ni binti wa pili wa mwalimu na mtumishi wa Mungu, Christopher Mwakasege na mama Diana Mwakasege.

 

 

Anna alipata maono ya kuwa rubani akiwa darasa la 3 tu na baba yake, Mwalimu Mwakasege alikuwa naye bega kwa bega kuhakikisha ndoto zake zinatimia. Ni baba yake huyu ndiye ambaye kwa mara ya kwanza alimpeleka uwanja wa ndege angalau akaione ndege ‘live’ badala tu ya kuziona angani tu zikipita.

 

 

Alipofika darasa la 5, baba yake alimtembeza uwanja mdogo wa ndege Arusha ambapo alipata nafasi ya kuzungumza na marubani kuhusu ndoto yake, nao wakampa ushauri masomo ya kusoma ili aweze kuifikia ndoto hiyo.

 

 

Siku zilizidi kusonga mbele huku Anna akiendelea kuifukuzia ndoto yake, hatimaye akahitimu masomo yake hapa nchini na kuelekea nchini Afrika Kusini ambako huko ndiko alikopata mafunzo ya urubani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad