“Mnachanga msibani wakati marehemu haongei” RC Gabriel akiwa Chato



RC Geita amehitimisha ziara yake Chato kwa kushiriki kwenye kuchimba Msingi wa madarasa 4 na ofisi 2 kwenye ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kitela ambayo wananchi wameamua kuijenga ili kupunguza msongamano shule ya Sekondari Chato yenye wanafunzi zaidi ya 2000.

Akizungumza na wananchi kwenye ujenzi wa Shule hiyo Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza Wilaya ya Chato kwa kuanza kutekeleza maagizo yake mapema kabla ya kuhitimisha ziara yake kwa kuanza kutatua kero ya msongamano wa wanafunzi kwa kuanzisha ujenzi kwa kushirikiana na wananchi.


“Katika wilaya zote nne nilizotembelea nilisema nitarudi kuxinfua kampeni ya ujenzi wa miundombinu kwenye zahanati na shule zetu, Chato mmenifurahisha sana kabla sijaondoka nimeshazindua kazi hii hapa,..nanyi wananchi nawaomba tusirudi nyuma tuendelee na moyo huu,” RC Gabriel


Vilevile, Mkuu wa Mkoa pamoja na mambo mengine amewataka viongozi wa Wilaya ya Chato kupitia Idara ya Ardhi kuhakikisha wanamaliza migogoro yote ya ardhi kwa kupima maeneo ya Vituo vya kutolea huduma za Afya wilayani humo na kutoa hati za umiliki kwa faida ya sasa na badae.


Mkuu wa Mkoa ameshafanya ziara wilaya za Mbogwe, Bukombe, Nyang’hwale na Chato na hivi karibuni ataanza wilayani Geita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad