LITIKISA kiberiti! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia staa wa Bongo Fleva na Mwanamitindo Hamisa Mobeto kushindwa kutimiza azma yake ya kumburuza mahakamani, Muigizaji Kajala Masanja licha ya kujinasibu kufanya hivyo.
Mobeto kupitia kwa wakili wake, alimuandikia barua ya Kajala akimtaka amuombe radhi la asipofanya hivyo atamfikisha mahakamani kwa kosa la kumchafua mitandaoni.
Mobeto alifikia hatua hiyo hivi karibuni mara baada ya Kajala kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa Mobeto amehusika katika kumtorosha binti yake kwenda kwa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ ambaye baadaye alisambaza picha za faragha na binti huyo wakifanya yao.
Waraka wa Kajala kwenda kwa Mobeto ulisomeka hivi:“…ilikuwa tarehe 9 saa 6 mchana Hamisa Mobeto aliniomba kutoka lunch na mwanangu, sikuona haja kumkatalia kwa sababu nilijua yeye ni mzazi ambaye ana mtoto pia wa kike, kumbe ndio hiyo siku ‘alitake advantage’ kwenda kumkutanisha na Rayvanny kwa manufaa yake binafsi.
“Walimrubuni mtoto mdogo kwa kumnywesha pombe, wamemrecord video chafu sawa mimi ni mnyonge siwezi wafanya chochote basi hata muogopeni Mungu kama Mungu hamumuoni, hamuiogopi Serikali?
“Na kuvujisha video bila woga wakati ni mtoto mdogo anasubiria mwezi wa 6 kuingia form 5 siamini kama kuna aliye juu ya sheria katika taifa hili kama lengo lilikuwa ni kudate mtoto mdogo ili kutimiza matendo haya machafu ya kustaajabisha haitoshi mnampatia mtoto pombe na kumrecord video chafu lengo lilikuwa nini kama sio kuharibu maisha ya msichana wa Kitanzania?….
”Mara baada ya Kajala kuandika waraka huo, mbali na kumtaka amuombe radhi, Mobeto alimtaka afute waraka huo aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram lakini hata hivyo Kajala hakufuta.
Taarifa za ndani kutoka kwa mtu wa karibu na Mobeto zimeeleza kuwa, Mobeto alishikwa pabaya na Kajala kwani alikuwa na ushahidi mwingi wa siku ya tukio na ndio uliomfanya Mobeto awe mpole.
“Mobeto ameoneshwa mpaka video za hoteli siku ya tukio hivyo akaona mambo yasiwe mengi asijishebedue kumfungulia kesi Kajala wakati ngoma itamgeukia yeye,” alisema mtu huyo wa karibu.
Mtu huyo alisema, kwa sasa Mobeto kwa kushirikiana na uongozi wa Rayvanny upo kwenye mchakato wa kuzima msala wa kusambaza picha chafu mtandaoni uliokuwa unamkabili Rayvanny pamoja na Mobeto mwenyewe.
Hivi karibuni alipotafutwa Kamanda wa Polisi Kinondoni, Ramadhan Kingai alisema sakata hilo bado lipo kwenye himaya yao, wanaendelea na uchunguzi kabla ya kulifikisha suala hilo mahakamani.
Amani lilimvutia waya Mobeto kupitia simu yake ya mkononi lakini iliita muda mrefu bila kupokelewa.
Stori: Mwandishi Wetu, Amani