Mshukiwa mmoja mwenye umri wa miaka 27 alikamatwa mjini Christchurch, New Zealand kwa madai ya kutishia kushambulia misikiti.
Wakati utambulisho wa mshukiwa huyo haukutangazwa, Mkaguzi wa Wilaya ya Canterbury John Price alisema,
"Ningependa kusema kwamba tunashughulikia maswala haya kwa umakini zaidi na tunafanya kazi ukaribu sana na jamii yetu ya Waislamu."
Price alitangaza kuwa kompyuta ya mtu asiyejulikana ambaye alitishia kushambulia misikiti kwenye mtandao ilikamatwa.
Mkaguzi wa Wilaya aliongezea kusema,
"Tishio lolote kwa jamii yetu na watu wetu halitapuuziwa. Ujumbe wowote wa chuki au mtu yeyote ambaye anataka kudhuru jamii yetu atahukumiwa."
Price hakutoa taarifa zaidi juu ya maelezo ya vitisho vilivyotolewa na mshukiwa huyo mtandaoni.
Shambulizi la kigaidi la silaha lilitekelezwa kwenye misikiti ya Nur na Linwood huko Christchurch, New Zealand siku ya Ijumaa tarehe 15 Machi 2019.
Gaidi Brenton Tarrant, aliyewaua watu 51 na kujeruhi wengine 49 katika shambulizi hilo, alihukumiwa kifungo cha maisha mnamo Agosti.