Mwambusi Aingia Anga za Gomes





KATIKA kuhakikisha kikosi chake kinakuwa imara na tishio katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi ameongeza program ya mazoezi ya gym.

 

Yanga imepanga kufanya vema msimu huu ikiwemo kubeba makombe yote wanayoshindania ikiwemo ligi na FA ambayo yote yanatetewa na Simba.

 

Program hiyo ya gym ambayo Yanga wameianza ndiyo inayotumiwa hivi sasa na Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes katika kukisuka kikosi chake kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Spoti Xtra, lina taarifa za kambi ya Yanga iliyopo Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Dar es Salaam chini ya Mwambusi ambaye ameongeza program ya mazoezi katika kuwaweka fiti nyota wake.



Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata gazeti hili, Mwambusi ameongeza program hiyo wanayoifanya asubuhi, huku jioni wakifanya mazoezi ya kimbinu uwanjani.

 

“Timu tangu imerejea kambini mara baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu Kaze (Cedric) aondolewe imekuwa ikifanya mazoezi kwa program moja pekee ya uwanjani saa kumi jioni. “

 

Lakini kocha Mwambusi tangu alipopewa timu alianza na mazoezi ya kuchezea mpira na kukimbia mbio fupi na ndefu muda wa jioni na hiyo ni katika kutengeneza fitinesi ya wachezaji.

 

“Lakini juzi walipoingia tena kambini, kocha ameongeza program ya gym itakayokuwa inafanyika kila siku asubuhi. “Jioni kocha amepanga kuwapa program ya kuchezea mpira ikiwemo mazoezi ya kimbinu ya jinsi ya kufunga na kulinda goli wakati timu ikiwa imepoteza mpira,” alisema bosi mwenye cheo kikubwa Yanga.

 

Alipoulizwa Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Yanga, Hassani Bumbuli, kuzungumzia hilo, alisema: “Kama uongozi kila kitu kinachohusiana na ufundi tumemuachia kocha na sisi viongozi tunasimamia masuala ya kiutawala, kuhusu maandalizi ya timu yanakwenda vizuri katika kujiandaa na michezo ijayo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad