Ombi la Bobi Wine kuondoa kesi ya uchaguzi laahirishwa





Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi WineImage caption: Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine
Mahakama ya juu nchini Uganda imeahirisha ombi la Robert Kyagulanyi la kuondoa kesi aliyowasilisha kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais mwaka 2021.

Tume ya Uchaguzi ilimtangaza mshindi Rais Museveni wa chama cha NRM kwa aslimia 59% huku Kyagulanyi akipata asilimia 35.

Kesi hiyo imeahirishwa kufuatia ombi la mawakili wa Robert Kyagulanyi kwamba leseni yao ya kazi imemalizika tarehe 28 mwezi wa Februari mwaka 2021.

Jaji mkuu wa Uganda Alfonse Owiny Dollo anayeongoza Japo la majaji tisa amempatia wakili wa Kyagulanyi, Merdard Ssegona Lubega hadi saa kumi na moja leo awe amepata leseni yake kutoka kwa msajili wa mahakama.

Kesi hiyo itaendelea kesho Ijumaa saa tatu na nusu asubuhi ambapo mahakama kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wa ombi la Bobi Wine kuondoa kesi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad