Ushawahi kujistukia kwa nini unaonekana mzee sana kuliko umri wako? Au Ukijilinganisha na rafiki zako wenye umri kama wako wewe unaonekana Umri umeenda sana hata shikamoo haziishi? Basi Maadui Hawa hapa:-
Sigara
Kutokana na kiwango kikubwa cha sumu ziitwazo Free radicals(ROS) unazozipata kila unapo ingiza Pafu moja la sigara.
Sukari
Kutokana na Kuzalisha Free radicals nyingi wakati wa mchakato wake Oxidation na huhatarisha mwili kuingia kwneye msongo wa sumu ziitwazo Reactive Oxygen species (ROS).
Pia Sukari inakuhatarisha na Unene, Kisukari, shinikizo la damu, Pumu Vidonda vya tumbo, magonjwa ya homoni mabavyo vyote hivyo ni magonjwa yanayo chakaza mwili.
Tafiti moja iliyofanywa na Dr solomon hapo Muhimbili ilionesha kwamba sampuli ya damu kutoka kwa wagonjwa wenye kisukari ilipopimwa Kiwango cha Free radicals kwa kutumia Spectrophotometer ilionesha kwamba wagonjwa waliokuwa na athari kubwa za kisukari walikuwa na kiwango kikubwa sana cha sumu hizo free radicals. Moja ya sababu kubwa ni sukari kuwa nyingi kwenye damu. Kushuka kwa Free radicals kunaendana na kupunguza sukari.
Vyakula Vya wanga
Vyakula hivi Pia vinachangia sana Kuzeesha kwa kutuhatarisha na magonjwa ya lishe. Hasa kwa baadhi yetu ambayo kwa asilimia zaidi ya 95 ya jamii hatustahimili vyakula vya wanga na sukari kiwango kikubwa.
Mafuta ya Mbegu za Mimea na Vyakula vilivyo kaangwa kwa mafuta hayo
Mafuta haya yanakuhatarisha kupata Free radicals nyingi kutokana na udhaifu wake kwenye moto. Pia yana kiwango kikubwa cha omega 6 ambapo vyote hivyo ni vihatarishi vya maradhi ya lishe na kuzeeka haraka.
Pombe
Inadumaza seli za mwili, Seli za Ini kwa Upamoja tunaita Hepatic and systemic Insulin resistance. Hii inakuhatarisha na maradhi karibia yote ya Lishe.
.
Kwa asilimia zaidi ya 95 ukiweza kuepuka maadui hao utaweza kudhibiti kuzeeka haraka ukilinganisha na umri wako.