Pluijm Afungukia Kurejea Yanga SC




ALIYEWAHI kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Muholanzi Hans De Pluijm amesema kuwa hajafanya mazungumzo na kiongozi wa timu hiyo kwa sasa juu ya kurejea Jangwani huku akitoa masharti ya yeye kutua hapo tena.


Pluijm ni moja kati ya makocha walioipa mafanikio Yanga chini ya utawala wake ambapo kwa sasa tayari timu hiyo imefuta benchi lake lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na Mrundi Cedric Kaze raia wa Burundi.

Tetesi nyingi zimekuwa zikieleza kuwa miongoni mwa makocha ambao wanafikiriwa kurejea ndani ya kikosi hicho ni pamoja na Pluijm mwenye kadi ya uanachama wa Yanga.

Mholanzi huyo aliweza kufanya kazi na Singida United kwa mafanikio ya kuipeleka hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho na baadaye Azam FC ambapo huko hakudumu kwa muda.

 

Akizungumzia hilo, Pluijm alisema kuwa “Sina tatizo lolote na Yanga, mimi ni kocha ambaye kazi yangu ni kufundisha hivyo nipo tayari kurejea kuifundisha kwa masharti.

 

“Kwanza kabisa wanatakiwa kufanya mazungumzo ya ‘serious’ kama kweli wanahitaji kufanya kazi na mimi, kwani hizo tetesi zipo tu kila siku na siyo mara ya kwanza kuzagaa taarifa hizo.

 

“Uzuri mimi ninalifahamu vizuri soka la Afrika, hasa hilo la Tanzania kutokana na kuwahi kufundisha hapo nikiwa na Yanga, Singida United na Azam FC,” alisema Pluijm.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad