Polisi Mbeya yamshikilia raia kwa China kwa kuchapa viboko Watanzania




Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia raia wa China Xiao Yong (33) kwa tuhuma za kuwashambulia  kwa kuwacharaza viboko  madereva wawili kwa madai ya kutumia fedha walizopatiwa kupeleka wilayani Kyela kwenye mashine za mchezo wa kubahatisha.


Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Urlich Matei leo Jumanne Machi 30, amewataja  walioshambuliwa kwa viboko na kusababishiwa maumivu makali kuwa ni   Ramadhani Ulodi(27) na Omary Miraji 25)



Amesema awali jeshi lilipata taarifa kutoka katika mitandao ya kijamii zikionyesha raia wa Tanzania wakichalazwa viboko na ndipo walipanza kufuatilia na kubaini lilitokea katika Mtaa wa Meta, Kata ya  Mabatini Jijini hapa.



"Tulianza ufuatiliaji na kubaini Watanzania hao ambao ni waajiriwa wa Kampuni ya Bonanza,"amesema.



Matei amesema polisi hawajafurahishwa na kitendo hicho na kuonya raia wa kigeni kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa kuwapiga  waajiriwa wao badala yake wawafikishe katika vyombo vya dola.



Amesema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi na atafikishwa mahakamani uchunguzi wa kesi hiyo utakapokamilika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad