Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, na kutuma salamu za rambi rambi kwa mjane Janet Magufuli, serikali na watu wa Tanzania.
Rais Kenyatta amesema Magufuli alikuwa kiongozi wa Afrika mwenye maono. ‘Nimempoteza rafiki, mwenzangu na mshirika wa karibu, alisemahe said.
Rais Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ametangaza siku saba ya maombolezo kitaifa nchini Kenya kwa heshima ya hayati Rais John Magufuli.
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Bendera ya Kenya zitapeperushwa nusu mlingoti katika majengo yote ya serikali nchini Kenya na katika balozi zake nje ya nchi, hadi siku Magufuli atakapozikwa.