Rais wa Msumbiji awafuta kazi wakuu wa majeshi





Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amewafuta kazi wakuu majeshi wa ardhini na angani wakati nchi inapokabiliana na wanamgambo wa Islamic States katika kaskazini mwa nchi hiyo na uasi wa wanamgambo wanaohusishwa na chama kikuu cha upinzani.
Katika taarifa iliyotolewa usiku Alhamisi rais hakutoa sababu ya kumfuta kazi Ezequiel Isac Muianga, mkuu wa jeshi la ardhini, na Messias André Niposso, mkuu wa jeshi la anga.

Rais pia amemfuta kazi kamanda na naibu kamanda wa chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Marechal Samora Macheya.

Naibu kamanda wa Taasisi ya mafunzo ya juu ya masuala ya ulinzi pia alifutwa kazi.

Msumbuji imekuwa ikipambana na uasi katika mkoa wenye utajiri wa madini wa Cabo Delgado tangu Oktoba 2017.

Watu nusu milioni wamefurushwa makwao mwaka uliopita pekee.

Kundi la al-Ansar al-Sunna, ambalo linajulikana na wenyeji kama al-Shabab, limehusika na makumi ya mashambulio ya kigaidi ambayo yanakaidiriwa kuuwa mamia ya watu.

Shirika la kutete haki la Amnesty International mwezi huu lilichapisha ripoti inayolaumu majeshi ya Msumbiji wajenzi wa majeshi wa kibinafsi na waasi wanaohudumu katika mkoa wa Cabo Delgado kwa kutekeleza uhalifu wa kivita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad