Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameishtumu Facebook kwa "ubabe", baada ya Facebook kumfungia akaunti yake kwa madai ya kwamba anaeneza habari za uongo kuhusiana na virusi vya corona.
Maduro akiituhumu Facebook kwa "Udhalimu wa Dijitali" kupitia mtandao wa Twitter amesema kuwa,
"Kwa kudhibitiwa kwa ukurasa wangu wa kibinafsi wa Facebook, nitaendelea kutuma maoni yangu ya kila wiki kuhusiana na Covid-19 kwenye ukurasa wa Facebook 'ConCiliaFlores', Instagram, Youtube na Twitter. Hawawezi kutufungia!"
Kulingana na Facebook, Maduro alikiuka sera za jukwaa hilo kwa kusambaza habari kuhusu utumiaji wa dawa "Carvativir", ambayo anadai ni nzuri dhidi ya Covid-19.
Facebook imefunga akaunti yake kwa muda wa siku 30.
Kwenye video hiyo iliyoondolewa na Facebook, Maduro alitaja dawa ya Carvativir iliyotengenezwa kwa mmea wa thyme kuwa kama "muujiza" na kudai kuwa inaweza kutumika katika kuzuia na kutibu virusi vya corona.