Rais wa zamani wa Somalia afariki nchini Kenya





Ali Mahdi Mohamed alikuwa rais kutoka mwaka 1991 hadi 2000Image caption: Ali Mahdi Mohamed alikuwa rais kutoka mwaka 1991 hadi 2000 Rais wa zamani wa Somalia afariki nchini Kenya
Rais wa zamani wa Somalia, Ali Mahdi Mohamed, amefariki siku ya Jumatano katika hospitali moja nchi jirani ya Kenya akiwa na umri wa miaka 82.

Alingia madarakani mwaka 1991 baada ya ra Rais Siad Barre kung'olewa madarakani na kusalia madarakani hadi mwaka 2000. Nafasi yake baadae ilichukuliwa na Abdiqasim Salad Hassan.

Rais Mohamed Abdullahi Farmajo ameagiza bendera zote nchini kupeperushwa nusu mlingoti kwa siku tatu kwa heshima ya rais huyo wa zamani.

Kamati ya kitaifa ya mazishi imeteuliwa, Bw. Farmajo amesema.

Wanasiasa na maafisa wa zamani wa serikali wamekuwa wakituma risala za rambi rambi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad