Na Maridhia Ngemela -Mwanza.
Waandishi wa habari wa kike mkoani Mwanza wamekemea vikali vitendo vya ya ngono kutoka kwa baadhi ya waajiri kuwataka kimapenzi wanawake wanaoenda kutafuta kazi katika ofisi zao.
Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari wanawake Mwenyekiti wa Jukwaa la waandishi wa habari za Utalii kanda ya ziwa Rose Jacob,walipotembelea mrdi wa Isanginjo Satellite City ambako kuna kiwanja cha Chama Cha Waandishi wa habari mkoani Mwanza (MPC)uliopo wilayani Magu mkoani Mwanza,ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.
"Tunaomba waandishi wa habari,wanawake wasikubali kutoa miili yao kwa ajili ya kupatiwa ajira,jambo ambalo linasababisha kutokuheshimika na kudhalilika kwa wanawake ikiwa na kupoteza ajira hiyo uliyoipata kwa ajili ya kutoa ngono,"alisema Rose.
Aidha katika Maadhimisho hayo waandishi hao walifanya harambe na kukusanya mifuko mia ya Saruji kwaajili ya kuanza ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Waandishi wa habari mkoani hapa.
Kwa upande wake afisa mchunguzi mwandamizi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa (takukuru )mkoa wa Mwanza dawati la elimu kwa umma, Maua Ally alisema wanawake wajiamini ,wajitume na wasisite kutoa taarifa ya viashiria vya rushwa ya ngono wanapokutana na changamoto hizo.
Alisema mwanamke akijiamini na kufanya kazi kwa jitihada kwa kufuata sheria na haki ni virahisi kukwepa rushwa ya ngono na kuikemea kiujumla hata kuwa mfano kwa wengine.
Wasaidizi wa kazi za ndani wanaopata mafunzo kutoka shirika la wote sawa kwa nyakati tofauti walisema vitendo vya rushwa vipi majumbani hususani kutoka kwa waajili ya kiume na watoto wa familia husika na kusababisha kutodumu kwenye kazi zao ili kukwepa adha hiyo ya rushwa ya ngono .
Mkurugenzi wa shirika la wote sawa Angela Benedictor alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani katika viwanja vya furahisha alisema kuwa,waajiri wa kike wapunguze unyanyasaji wa wasaidizi wa kazi za ndani na kuishi nao vyema ili kuweka usawa kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema kuwa wanawake katika uongozi chachu kufikia dunia yenye usawa.