Shujaa wa Kenya Westgate 'aungwa mkono kwa kiti cha seneti'





Mfanyabishara Abdul Haji, aliyepata umaarufu kwa kukabiliana na wanamgambo waliovamia duka la Westgate katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, mwezi Septemba 2013, ameidhinishwa kumrithi baba yake Yusuf Haji kuwa seneta wa Garissa, gazeti la Standard limenukuu taarifa ya familia yake.
Wakati wa shambulio hilo, Bw Haji aliingia ndani ya duka hilo kumtafuta ndugu yake akiwa amejihami kwa bastola tu ambayo alifundishwa na baba yake kutumia kwa uwindaji alipokua mtoto.

Akiwa pamoja na kundi dogo la maafisa wa polisi waliokuwa wameavalia nguo za nyumbani, alisaidia kuokoa makumi ya watu kutoka kwenye duka hilo.

Familia yake sasa limemuidhinisha kukamilisha muhula wa pili wa baba yake katika bunge la seneti, gazeti hilo liliripoti.

Seneta Haji alifariki mwezi uliopita mjini Nairobi na uchaguzi mdogo umepangiwa kufanyika mwezi Mei.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad