Shule Iliyoburuza Mkia Miaka Mitatu Yafanya Maajabu




Shule ya Sekondari Kome iliyoko Halmasahauri ya Buchosa Wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza iliyoshika nafasi ya mwisho kwa miaka mitatu mfululizo kwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne na chapili imeongeza ufaulu kwa matokeo mazuri ya mwaka 2020 kwa vidato vya mtihani kwa asilimia 88 kidato cha nne na asilimia 97 kwa kidato cha pili.

 

 

Shule ya Sekondari Kome nimiongoni mwa shule 20 za Sekondari ziliko halmashauri ya Buchosa ambayo imekuwa na matokeo mabaya kwa miaka mitatu mfululizo kutokana na usimamizi mbovu wa mkuu wa shule aliyekuwepo.

 

 

Kutokana na hali hiyo ofisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Buchosa Bruno Sangwa alifanya uamuzi wa babadiliko ya uongozi na kumtoa aliyekuwa mkuu wa shule hiyo Lukas Lupimo na kumpeleka aliyekuwa mkuu wa shule ya Sekondari Bukokwa Dunia Luhula na shule hiyo kuanza kupata matokeo mazuri.

 



Miaka mitatu mfululizo shule hiyo ilishika nafasi ya mwisho ambapo mwaka 2017 ilishika nafasi ya mwisho kiwilaya kati ya shule 20 na kimkoa ilikuwa nafasi ya 195 Kati ya shule 242, mwaka 2018 ilishika nafasi ya mwisho kiwilaya kati ya 20 na kimkoa ilishika 242 Kati ya shule 242 na mwaka 2019 ilishika nafasi ya mwisho kiwilaya kati ya shule 20 na kimoka lishika nafasi ya mwisho 241 Kati ya shule 241 Mkoa mwanza.

 

 

Kwa mwaka 2020 hali imekuwa tofauli kutokana na kuongeza ufaulu ambapo kwa matokeo ya kidato cha nne imeshika nafasi ya 14 Kati ya shule 20 huku kimoa ikishika nafasi 195 ya Kati ya shule 241 huku matokeo ya kidato cha pili imeshika nafasi ya 9 Kati ya shule 20.

 

 

Shule ya Sekondari Kome inaidadi ya wanafunzi 1026 walimu 15 vyumba vya madarasa 11 ,mahitaji vyumba 23 pungufu vyumba 12.

 

 

Mkuu shule ya Sekondari Kome Dunua Luhula alisema yeye alihamishiwa kwenye shule hiyo mwaka mwezi februari 11/ 2020 na lipofika alikutana walimu hawawajibika na kufumua mfumo mzima na kumeza matunda.



 

Siriya mafaniko

Alisema Siri ya mafaniko ni mwalimu kukubali kukukosoa kutokana na mapungufu waliyonayo kiutendaji ,nidhamu kwa walimu na na wanafunzi pamoja na Wazazi ,idara ya taaluma kusimaamia vema majuku yao kikamilifu juu ya mazozi ya Kila siku kwa wanafunzi.

 

 

“Kuanzia mwaka 2021 mipango yety nikuhakisha shule hiyo inashika nafasi za juu kiwilia na Kimkoa na kuhakikisha wanatokomeza Zero kwenye shule hiyo” alisema Luhula.

 

 

Mwili wa Taaluma kwenye shule Bagini Simon alisema matokeo mabaya yaliyokuwa yanapatikana kwenye shule hiyo kwa miaka mitatu mfululizo yalitokana na usimamizi mbovu wa mkuu wa shule aliyekuwepo kuwa tofauti na walimu wenzake , pia utoro wa wanafunzi , wanafunzi kuchelewa shule kutokana na umbali mrefu kufika shule kutokana na kutemba kwa umbali wa kilometa 7 hadi 10 kufika shuleni.

 

 

Bagini alisema kwa Sasa wanawajengea uwezo wanafunzi wa kujiamini wanapokuwa wakifanya mitihani hiyo nikutokana na kuwapatia mazoezi ya mara kwa Mara ili waweze kujitegemea.

 

 

“Mimi kama mkuu wa idara ya taaruma nitahakisha idara yangu unawatendea vema wanafunzi lazima wafaulu tutatokomeza zero,”alisema Bagini.

 



Anna simoni mwanafunzi anayesoma kome sekindari kidato cha pili alisema kwa Sasa walimu wanamejitoa kufundisha tokana na uongozi kubadilisha na wamekuwa kitu kimoja tutajitahidi na tutasoma kwa bidii nahatiye kufaulu mtihani.

 

 

Mmoja wa Wakazi wa Kijiji cha Nyakasasa Juma Tulubuza alisema madabiliko ya uongozi yameleta uahuweni kwenye shule hiyo ambayo Wazazi walikuwa wametakata taama kupeleka watoto wao kutokana na matokeo mabaya yalikowa kwenye shule hiyo.

 

 

Usuli

Madiliko ya uongozi yaleta ongozeko la ufaulu Kome Sekondari iyokuwa imeshika nafasi ya mwisho kwa miaka mitatu mfululizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad