Dakika 45 za kipindi cha Kwanza zilikuwa za jasho kwa Simba mwenyeji wa mchezo dhidi ya Prisons, unapendelea Uwanja wa Benjamin Mkapa,Dar es Salaam.
Hii ni mechi ya mzunguko wa pili, baada ya kwanza Simba kuchapwa bao 1-0 ugenini.
Mechi imeanza kwa ushindi mkali, si Simba wala Prisons zilikuwa zinasaka kupata bao, lakini imeshindikana dakika 45 za kwanza.
DAKIKA 20 ZA MWANZO
Ndani ya dakika 10 hakuna timu iliofanikiwa kulenga golini, huku washambuliaji wa Simba wakabiwa nje ya 18.
Jambo lililowalazimu mawinga Larry Bwalya (dakika ya 8) na Luis Miquissone (dakika ya 12) kupiga mashuti ya mbali hata hivyo waliyapaisha.
Dakika ya 11 Jeremiah Juma alipiga shuti lililolenga langoni kwao Simba na Aishi Manula alikuwa makini kuudaka mpira.
Wachezaji wa Prisons hawaonyeshi uoga wa kucheza ugenini, jambo linalowapa changamoto mastaa wa Simba kusaka njia ya kupenya wa kwenda mbele kushambulia.
Wakati mpira unaanzishwa dakika ya kwanza mchezaji wa Prisons, aliupiga mpira nje kama mara tatu hivi.
DAKIKA 23 HADI 45
Dakika ya 27 beki wa kati wa Prisons, Vedastus Mwihambi alishika mpira katika purukushani za kuzuia mashambulizi ya Chriss Mugalu, mwamuzi akaamuru ipigwe penalti.
Mugalu ndiye aliyepiga penalti hiyo, iliyookolewa na kipa Jeremiah Kisubi kwa kuipangulia nje.
Kukosa penalti kwa Mugalu ni kama kuliendelea kuwapa nguvu wachezaji wa Prisons kujituma zaidi.
Dakika ya 34 kocha wa Prisons alifanya mabadiliko ya kumtoa Nurdin Chona ambaye aliingia na nafasi yake ikachukuliwa na beki namba mbili Doto Shaaban.
Kadri muda ulivyokuwa unayoyoma, wachezaji wa Prisons walianza kurudi nyuma kujilinda baada ya Simba kusoma njia ya kufika langoni kwao.
Dakika ya 42 mchezaji wa Prisons, Jumanne Elfadhil alipata kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Mugalu.
Kikosi cha Simba kipa ni Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohamed Hussein'Tshabalala', Joash Onyango, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Paferct Chikwende, Mzamiru Yassin, Chriss Mugalu na Luis Miquissone.
Waliopo benchi ni Beno Kakolanya, Erasto Nyoni, Thadeo Lwanga, Bernard Morrison, Meddie Kagere, John Bocco na Clatous Chama.
Kikosi cha Tanzania Prisons kipa ni Jeremiah Kisubi, Salum Kimenya, Benjamin Asukile, Vedastus Mwihambi, Nurdin China, Jumanne Elfadhil, Ezekia Anderson, Lambart Charles, Samson Baraka, Jeremiah Juma na Adili Buha.
Waliokuwa benchi ni Prosper Kaini, Doto Shaaban, Seleman Mangoma, Gasper Mwaipasi, Marco Mhilu, Kassim Mdoe na Mohamed Mkopi.
Waamuzi ni wakati Emmanuel Mwandembwa (Arusha), MC :Khalid Bitebo (Mwanza), msaidizi wa kwanza ni Abdulaziz Ally (Arusha) na msaidizi wa pili ni Isihaka Mwalile( Dar es Salaam).