Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika, klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al-Merrrik ya Sudan kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa makundi wa michuano hiyo na kuhitaji alama moja tu ili kutinga hatua inayofuata ya robo fainali.
Mabao ya Simba, yamefungwa na Jose Luis Miquissone dakika ya 19, Nahodha msaidizi Mohamed Hussein akifunga bao la pili huku Chris Mugalu akikamlisha ulinzi wa ushindi huo kwa kufunga bao la tatu dakika ya 49 ya mchezo.
Simba imeendelea kusalia kileleni mwa kundi A kwa kufika jumla ya alama 10, Al Ahly ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 7 baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AS Vita ugenini na kuwaacha AS Vita nafasi ya tatu wakiwa na alama 4 huku Al Merrick akishika mkia akiwa na alama 1 pekee.
Simba inatazamiwa kushuka tena dimbani tarehe 2 mwezi Aprili 2021 kukipiga na AS Vita kwenye dimba la mkapa huku ikitafuta alama pekee kujihakikishia kufuzua hatua ya robo fainali kabla ya kumaliza mchezo wa mwisho wa makundi kwa kucheza na Al Ahly tarehe 9 April 2021 nchini Misri.