Tanzia: Nabii Bushiri Ailaumu Serikali Kifo cha Mwanaye





MHUBIRI maarufu wa Afrika wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering (ECG) la kutoka Malawi, Shepherd Bushiri, ametangaza kifo cha binti yake Israella mwenye umri wa miaka nane.

 

 

Bushiri, ambaye kanisa lake linafuatwa na mamilioni kote Barani Afrika, hajataja sababu ya kifo cha binti yake lakini alisema kwamba madaktari wamemwambia maisha yake yangeokolewa ikiwa mamlaka ya Malawi haingemzuia kuondoka nchini humo kutafuta matibabu nchini Kenya.



Mnamo Februari, mamlaka ya Malawi ilizuia ndege ya kibinafsi iliyokuwa imebeba watoto wa Bushiri Raphaela na Israela, binamu yake Esther na mama mkwe Magdalena Zgambo kuondoka kwenda Kenya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu huko Lilongwe.Bushiri alisema wanafamilia hao wake walikuwa wakisafiri kwenda Kenya kutafuta msaada wa matibabu kwa Israella.
 

Serikali ya Malawi ilibadilisha uamuzi wake ndani ya siku chache baada ya timu ya mawakili ya Bushiri kwenda kortini, lakini Failia ya Bushiri iliamua kusitisha safari ya kwenda Kenya kabisa na waliendelea kutafuta msaada wa matibabu nchini Malawi.Akitangaza kifo hicho Jumatatu, Bushiri alisema kuwa hatakwenda kumlilia binti yake, lakini badala yake alitaka kusherehekea maisha yake.

 

‘Nabii’ Bushiri anaendesha Kanisa lake la ECG nchini Afrika Kusini lakini alikimbilia Malawi katika hali ya kutatanisha mnamo Novemba baada ya kukwepa dhamana wakati alipokabiliwa na mashtaka ya utapeli na utakatisaji fedha ncini humo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad