Uganda yaanza kampeni ya chanjo ya Covid-19





Uganda imeanza kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 siku ya Jumatano baada ya kupokea dozi 864,000 ya chanjo aina ya Oxford-AstraZeneca wiki iliyopita.
Waziri wa Afya Jane Ruth Aceng alikuwa wa kwanza kupokea chanjo hiyo katika hospitali kuu mjini, Kampala.

Waliopewa kipaumbele ni wahudumu wa afya nchini huku baadhi yao wakipanga foleni katika Hospitali ya Rufaa ya Mulago huko Kampala kuchanjwa.

Makundi mengine yamepangiwa kupokea chanjo ni maafisa wa usalama, waalimu na watu wazima walio na umri wa zaidi ya miaka 50 na watu walio na changamoto zingine za afya.

Kampeni ya chanjo itapelekwa katika vituo vya afya kote nchini katika kipindi za siku tano zijazo

Wale watakaochanjwa watapokea dozi ya pili ya chanjo hiyo katika miezi ya Mei na Juni.

Dozi zaidi za chanjo 2,688,000, chini ya mpango wa Covax inatarajiwa nchini humo ifikapo mwezi Juni.

Uganda inalengo la kutoa chanjo kwa asilimia 49.6% ya watu wake kwa awamu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad