Umoja wa Mataifa umesema Virusi vya Corona vinasababisha vifo kwa Wanaume wengi zaidi Barani Afrika kuliko Wanawake ambao wao wanaandamwa na kupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi
Utafiti uliofanyika kwenye Nchi 28 za Afrika, ikiwemo #Guinea, #Mauritius na #Uganda umeonesha kwa wastani idadi ya Wanawake waliopata maambukizi au kufa kwa corona ni ndogo ikilinganishwa na Wanaume
Takwimu zinaonesha asilimia 41 ya Wanawake Barani Afrika ndiyo wamekumbwa na Janga la Corona lakini idadi hiyo inatofautiana miongoni mwa Mataifa
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti amesema kwa Wanawake janga la COVID19 limesababisha ukosefu wa huduma za uzazi