Lazima tukubali huu utatu wa mameneja wa WCB wanafanya kazi yao kwa weledi mkubwa.
Ni ukweli usiopingika hata wewe unaesoma hapa, mtoto wako akiwa na kipaji kikubwa cha kuimba. Ukiambiwa umtafutie management serious ya kumpa mafanikio huu utatu ndio utakuwa wa kwanza kuja kichwani mwako.
Nataka niwaonyeshe matukio machache ya hivi karibuni ili muone awa jamaa wanaijua kazi yao hawabahatishi
Tukio la Rayvanny na Paula; Mpaka tukio linaisha hatukuona picha yoyote ya Rayvanny akiwa maeneo ya polisi, japo tunaambiwa alikaa kwa muda rumande. Hii haijatokea bahati mbaya kuna watu wamefanya kazi yao kulinda image ya msanii wao. Hata wale walazimisha kiki walipojaribu kuchokonoa Instagram na redioni hawakupata reply yoyote, walipuuzwa.
Tukio la Superwoman; we all know kumpata makamu wa rais kwenye tukio la media iliyotoka kufungiwa sio kitu kidogo, tena tukio lilifana mpaka wengine wakadhani Superwoman ni kampeni ya kitaifa. Yote haya hayajatokea bahati mbaya kuna watu wanafanya kazi yao.
Tukio la uzinduzi wa label ya Rayvanny; Wengi wamestaajabu namna management ya Wcb walivyompa support kijana wao, walitegemea wazo la kuanzisha kampuni yake ya music la Chui lingezua vita, ila imekuwa tofauti kapata ile support unaona kabisa imetoka na baraka. Hii pia sio bahati mbaya, wanajaribu kukuza brand ya Rayvanny na kutanua biashara yao. Who knows maybe keshokutwa kunaweza kusiwe na Wasafi as a music label bwana Chibu akaachia mambo ya usimamizi wa muziki kwa Ray.
Tukio la Shilole na shabiki wake mfaransa; kwenye lile tukio unaona kabisa Shishi alikula mpunga kwa yule demu na akamuaminisha anammudu Chibu. Bahati mbaya alimvamia Chibu sehemu isiyo sahihi kibiashara, watu wapo kwenye branding ya tukio lao yeye akawachanganyia tukio. Lakini pamoja na kuwa hawakupenda walijitahidi kuplay very smart wasichafue image yao.
Tukio la uzinduzi wa album ya Mbosso; album ya Mbosso inazinduliwa Jumamosi pale Mlimani city kiingilio cha juu ni mil 5 kwa meza za VVIP na kiingilio cha chini ni elfu 50. Viingilio vinaonekana ni vikubwa lakini nawahakikishia tukio litakuwa sold out na pale Mcity hapatakuwa na pakukanyaga. It's all about branding and perception.
Keshokutwa usishangae kumuona Lavalava nae ana jambo lake.
Albums, EPs, hitsongs, corporate events, mwisho wa mwaka wakifunga hesabu rotation ya muziki inabaki WCB na si kwa bahati mbaya