Wachezaji wanne wa Harambee Stars kukosa baada ya kupatikana na Covid-19





Michael Olunga ni miongoni mwa wachezaji wa Harambee Stars waliopatikana na virusi vya coronaImage caption: Michael Olunga ni miongoni mwa wachezaji wa Harambee Stars waliopatikana na virusi vya corona
Wachezaji wa Harambee Stars Nahodha Michael Olunga, Mlinzi Joash Onyango, kiungo wa kati Lawrence Juma na mlinda lango Ian Otieno watakosa mchuano wao w akirafiki dhidi ya Togo hivi leo baada ya kupatikana na virusi vya Corona

Hatua hiyo imemlazimu Kocha Jacob Mulee kukifanyia mabadiliko kikosi chake kitakachoshiriki mchuano huo kwneye uwanja wa State de Kegue .

Masud Juma sasa ataongoza safi ya ushambuliaji huku Wing’a wa Gor Mahia Clifton Miheso akimpiga jeki kwa upande wa kushoto .

Kiungo wa kati wa Bandari Abdallah Hassan, aliyefunga bao la pekee katika sare ya bao moja waliotoka na Misri siku ya Alhamisi atakuwa katika upande wa kulia .

Kevin Kimani wa klabu ya Wazito atashirikiana na Duke Abya na Duncan Otieno katika safu ya kati.

Mchezaji wa AFC Leopards Clyde Senaji, aliyechukua nafasi ya Kenneth Muguna, anaichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza na atakuwa katika safu ya nyumba pamoja na wenzake Erick 'Marcelo' Ouma, Nahashon Alembi wa KCB na Daniel Sakari wa Kariobangi Sharks.

Kipa wa Ulinzi Stars James Saruni pia anavalia jesi ya taifa kwa mara ya kwanza kuichukua nafasi ya Ian Otieno wa Zesco United .

Ushindi kwa Stars utawawezesha kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi G.Viongozi wa kundi hilo Misri na Comoros tayari wamejikatia tiketi katika mechi hizo za ubingwa wa bara Afrika

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad