Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, imeendesha operesheni kupitia waganga wa jadi kutoka Shinyanga na kufanikiwa kuwaua fisi 11.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni wiki mbili baada ya fisi kuuwa watoto watatu na kujeruhi watu zaidi ya wanane.
Pia wameweka mpango wa kuanza operesheni kwa ajili ya kuwasaka fisi wanaofugwa majumbani.
Mkuu wa Wilaya hiyo Wilson Shimo amesema waliamua kutumia waganga wa jadi kusaka fisi hao, kwa sababu wanahusushwa na imani za kishirikina.