Baadhi ya waganga wa tiba asili mkoani Mtwara, wameiomba serikali kuthamini mchango wao huku wakilalamikia suala la usajili na kuomba kuruhusiwa kupeleka dawa zao zilizothibitishwa kutumika hospitalini ili kuokoa maisha ya watu hasa wenye matatizo ya upumuaji.
Kauli hiyo wameitoa mbele ya Mkuu wa mkoa huo Gelasius Byakanwa, wakati akizungumza na waganga hao na kuwasihi Watanzania kuacha tabia ya kutegemea mataifa ya nje katika masuala ya utafiti na badala yake wawatumie waganga wa tiba asili hasa katika kipindi hiki cha magonjwa ya mlipuko kwani waganga hao wanazo dawa za kutibu magonjwa ya mfumo wa hewa na upumuaji.
Wiki moja tangu mkuu wa mkoa huo kutoa tangazo la kuonana na waganga wa tiba asili, jumla ya waganga 41 kutoka maeneo mbalimbali wamejitokeza kwa ajili ya utambuzi wa dawa zao.