No title


WAMILIKI 736 mkoani Mwanza ambao ni wadaiwa sugu wa kodi ya aridhi wamefikishwa katika Baraza la Mahakama ya Ardhi na Makazi ili kujibu tuhuma za kushindwa kulipa kodi kwa zaidi ya miaka miwili hadi kumi kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi inavyoelekeza.

 


Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, leo Ijumaa, Machi 12, 2021, Kamishina wa Ardhi msaidizi wa Mkoa wa Mwanza, Elia Kamihanda, alisema kutokana na wadaiwa sugu 736 wa deni la ardhi kushindwa kulipa kiasi cha Sh Bilioni 3.3, wameamua kuwafikisha mahakamani jana Machi 11.

 
 

“Kwa mjibu wa sheria ya ardhi kama mmliki akipokea hati ya kumtaka kulipia deni lake ndani ya siku 14 na akishindwa, Kamishina wa ardhi amepewa haki ya kumfikisha mahakamani mdaiwa ndani ya siku hizo, maana wapo wanaodaiwa miaka miwili na kuendelea,alisema Kamihanda.


 

Wadaiwa hao ni kutoka wilaya za Nyamagana, Misungwi, Magu na Ilemela, ambako jumla ya kesi ni 11000 zenye gharama ya Bilioni 12, kati ya hizo kesi 736 ndiyo zimefikishwa mahakamani kwa awamu ya kwanza.


 

Aidha kesi hizo zaidi ya 700 zilifikishwa katika baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Mwanza, lilokuwa na mwendesha mashitaka Elia Kamihanda (Kamishina Msaidizi mkoa) na Mwenyekiti wa Baraza hilo Magambo Mayeye.

 

 

Kwa mjibu wa kifungu cha 50 cha sheria ya ardhi, kimeweka bayana endapo mmiliki akipewa hati ya madai ndani ya siku 14 basi ofisi ya kamishina inajukumu la kumfikisha mahakamani ili ofisi ya ardhi ipewe kibali cha kukamata mali na kumfutia hati mdaiwa na atapewa mtu mwingine.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad