“Wanaume Fanyeni Tohara” Jafo

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka wanaume ambao hawajafanyiwa tohara katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara kuhakikisha wanajitokeza ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini.


Akizindua huduma ya tembezi tohara kwa wanaume leo mjini Dodoma, Jafo amesema kuna faida kubwa kwa wanaume kufanyiwa tohara.


“Hii ni fursa pekee na haijawahi kutokea katika maeneo mengi, Kanda ya Ziwa watumie fursa hii adhimu kujitokeza kwa wingi kufanya tohara tembezi,” Jafo.


Alisema mikoa 16 ambayo inachangamoto kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi ni kutokana na watu kutofanyiwa tohara.


Jafo amesema takwimu zinaonyesha kuwa wanaume waliofanya tohara wana asilimia 60 ya kujikinga na mambukizi ya virusi vya ukimwi, pia inapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya kaswende.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad