Jeshi la Polisi Kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya (ADU) limewakama watu wanne akiwemo mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA), Allu Mirumgwa (24) wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilo 31 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye mabegi mawili.
Mkuu wa Kitengo cha ADU,Hassan Kabeleke aliwataja watuhumiwa wengine ni Joseph Dalidali(26) mkazi wa Mbezi beach,Said Mbasha(24) mkazi wa Kinondoni na Fatuma Shomari
Akizungumza leo Jumanne Mkuu wa Kitengo cha ADU, Hassan Kabaleke amesema Machi 2,2021 walipokea taarifa kutoka Kwa raia mwema kuwa kuwa kuna watu wanajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya eneo la Mbezi beach na Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Amesema baada ya kupolea taarifa hizo walipanga timu tatu ya Askari ambapo walianza kufatilia Machi 3 mwaka huu huko maeneo ya Mbezi Beach A mtaa wa Madafu walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Dalidali alipohojiwa alikiri kukihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
"Mtuhumiwa Dalidali ambaye anamiliki gari aina ya Toyota tulipomuhoji alituambia dawa hizo zimehifadhiwa Kijitonyama mtaa wa Mpakani B siku hiyo hiyo tulienda hadi eneo hilo," amesema Kabaleke.
Kabaleke amesema Machi 3 mwaka huu saa 8 mchana walimkamata mwanafunzi wa chuo cha uhasibu, Murungwa akiwa eneo la Kijitonyama na alipekuliwa katika nyumba aliyokuwa amepanga na kukutwa na pakiti 31 zenye uzito wa kilo 30.6 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye mabegi mawili.
Amesema mtuhumiwa Murungwa alipohojiwa alikiri kuwa dawa hizo za kulevya aliletewa na mpenzi wake Mbasha ambaye anaishi Kinondoni A mtaa wa Kasaba.
Baada ya kuelezwa hivyo walienda na kufatilia ambapo walimkamata Mbasha nyumbani kwake Kinondoni A na alipopekuliwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi alikutwa na fedha taslimu Dola za kimarekani 14,000,Sh 13,261,000 pamoja na misokoto mitatu ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa gramu 2.63.
Kabaleke amesema wakati wanamkamata mtuhumiwa Mbasha ndani ya chJeshi la Polisi Kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya (ADU) limewakama watu wanne akiwemo mwanafunzi wa chuo cha uhasibu (TIA), Allu Mirumgwa (24) wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilo 31zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye mabegi mawili. umba hicho alikutwa Fatuma ambaye alikiri kuwa yeye ni mpenzi wake na begi moja lililotumika kuhifadhi dawa za kulevya ni la kwake.