Wasiopata Chanjo ya Corona Marufuku Kuingia Makka

 


TAIFA  la Saudi Arabia limesema waumini wa dini ya Kiislamu watakaoruhusiwa kuhudhuria Ibada ya Hijja mwaka huu 2021 wanapaswa kuthibitisha kuwa wamepatiwa chanjo dhidi ya virusi vya Corona.

Waziri wa Afya Nchini humo ameagiza maandalizi yafanyike kwa kuajiri wataalamu wa huduma ya Afya katika vituo vya afya huko Makka na  Madina na maeneo matakatifu.

Tahadhari hii ina maanisha waumini kutoka mataifa yatakayochelewa kutoa chanjo kwa watu wake huenda wakashindwa kuhudhuria ibada hiyo.

Kutokana na kusambaa kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwaka 2020 Saudia ilipunguza mahujaji hadi kufika 1,000 ambao waliruhusiwa kwenye Ibada hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad