Watu 5 wamefariki baada ya jengo kuporomoka Misri






Takriban watu 5 wamefariki baada jengo la ghorofa 9 kuporomoka katika eneo la Jisr al-Suez Mashariki mwa Cairo. Watu wengine zaidi ya 24 wamejeruhiwa. 


Mkuu wa utawala wa mkoa wa jijini Cairo, Khalid Abdel-Al amesema waokoaji wanaendelea kuwatafuta manusura walionaswa chini ya kifusi cha jengo hilo katika kitongoji cha el-Salam. Polisi waliweka utepe kufunga eneo kuwazuia watu walioonekana kuwatafuta jamaa zao. 



Hata hivyo haijabainika moja kwa moja ni nini kilichosababisha kuporomoka kwa jengo hilo. Ingawa kuporomoka kwa majengo sio jambo geni nchini Misri, Mara nyingi unalaumiwa utunzaji duni wa majengo ya zamani na ukiukaji wa kanuni za ujenzi. 



Waendesha mashtaka wa wilaya wameamuru kuundwa kwa kamati ya kiufundi kutathimini sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad