WHO imesema Hakuna sababu ya kusitisha kutumia chanjo ya AstraZeneca






Mataifa hayapaswi kusitisha matumizi ya chanjo ya corona ya AstraZeneca kwa kuhofia kusababisha kuganda kwa damu wakati hakuna ukweli wowote juu ya hilo, Shirika la Afya Duniani limesema.


Bulgaria, Denmark na Norway ni miongoni mwa mataifa ambayo yamesitisha matumizi ya chanjo hiyo.



Lakini Ijumaa, msemaji wa WHO amesema hakuna uhusiano wowote baina ya chanjo hiyo na hatari ya watu kuganda damu.



Margaret Harris amesema chanjo hiyo ni salama na iendelee kutumika



Watu wapatao milioni 5 barani ulaya tayari wamepata chanjo hiyo ya AstraZeneca.



Kuna kesi zipatazo 30 barani ulaya za watu kupata madhara ya kuganda damu baada ya kuchanjwa chanjo hiyo.



Kuna ripoti ya mwanamke mwenye umri wa miaka 50-aliyefariki baada ya kuganda damu alipopata chanjo hiyo.



WHO inafanyia uchunguzi taarifa hiyo, kama kuna maswali yeyote kuhusu usalama, Bi Harris alisema.



Lakini hakuna uhusiano wowote wa matatizo ya kiafya ulioripotiwa kutokana na chanjo hiyo, aliongeza.



Bulgaria imeamua kusitisha kutoa chanjo hiyo kama vile Denmark, Iceland na Norway pamoja na Thailand. Italia na Austria zimeacha kuendelea kutumia dozi hiyo pia kwa kuchukua tahadhari tu.



"Niliagiza kusitishwa kutolewa kwa chanjo ya AstraZeneca mpaka wakala wa dawa Ulaya atakapotuthibitishia mashaka yote yaliyopo juu ya usalama wa dozi hiyo," alisema waziri mkuu wa Bulgarian, Boyko Borisov .



Shirika la madawa la Muungano wa Ulaya(EMA) lilisema awali kwamba hakuna dalili kwamba chanjo hiyo inasababisha kugada kwa damu mwilini, likiongeza kuwa ni "faida ambayo zinaendelea kuwa kubwa kuliko hatari zake.



AstraZeneca ilisema kuwa usalama wa dawa umefanyiwa utafiti mkubwa katika majaribio ya tiba, ikiwa ni pamoja na katika maabara za Ureno, Australia, Mexico na Ufilipino ,wamesema kuwa wanaendelea na mpango wa utoaji wa chanjo.



Mataifa mengine ambayo yanataka kusitisha mi pamoja na Uingereza, Ujerumani ,Mexico na Australia.



Hakuna ushahidi unaohusishwa

Nchini Uingereza Shirika la udhibiti wa bidhaa za huduma za afya(MHRA) lilisema kuwa hapakuwa na ushahidi kwamba chanjo hiyo ilisababisha matatizo, na watu wananapaswa kuendelea kuchanjwa wakati wanapoombwa kufanya hivyo.



Zaidi ya dozi milioni 11 za chanjo ya AstraZeneca zimekwisha kutolewa kote Uingereza, kwa mujibu wa MHRA.



Ureno imesema kuwa faida za chanjo zinaendelea kuwa kubwa kuliko hatari zake kwa wagonjwa, na itaendelea kuitumia chanjo hiyo.



Imesema haijapata uhusiano wowote wa chanjo na kuganda kwa damu.



Australia, ambayo tayari imekwishatuma dozi 300,000 za chanjo ya AstraZeneca , imekuwa ikielezea uamuzi wake wa kuendelea kutumia chanjo ya AstraZeneca.



"Kwa sasa ushauri ambao ni wa wazi kutoka kwa madaktari ni kwamba hii ni chanjo salama na tunataka chanjo iendelee kutolewa.



Wizara ya afya ya Ufilipino pia imesema kuwa '' hakuna sababu'' ya kuzuia chanjo huko.



Korea Kusini pia inaonekana kuendelea na mpango wake wa utoaji wa chanjo hiyo, ingawa imeelezea hofu yake.



Takriban dozi 785,000 zimewasili nchini humo tayari.



Mamlaka nchini humo hivi karibuni zilisema kuwa vifo vinane vilivyotokea katika kipindi cha kupokea chanjo havikuhusina na chanjo.



Baadaye walibaini kuwa hapakuwa na uhusiano baina ya chanjo na vifo hivyo.



Hatahivyo , Denmark, Norway pamoja na Iceland zimesitisha kwa muda mpango wake wa utoaji wa chanjo.



Italia na Austria, wakati huo huo, zimeacha kutumia aina fulani ya chanjo hiyo kama hatua yake ya kuchukua tahadhari.



Katika taarifa ya awali, EMA ilisema kuwa uamuzi wa Denmark ulikuwa ni "hatua ya kuchukua tahadhari huku uchunguzi kamili ukiendelea kuhusu ripoti za ugandaji wa damu miongoni mwa watu waliopokea chanjo, likiwemo tukio moja nchini Denmark ambako mtu mmoja aliuawa ".



Hali ikoje Ulaya?



Baada ya maambukizi kupungua katika miezi ya hivi karibuni katika mataifa mengi barani Ulaya.



Ufaransa, Italia ,Poland na Uturuki zimeonekana kuwa na idadi ya juu ya maambukizi katika wiki za hivi karibuni.



Italia imeweka marufuku mpya kwa kuweka kafyu wakati wa mapumziko ya Pasaka tarehe 3 mpaka Aprili 5 .



Chini ya muongozo uliodhibitishwa na serikali , wakazi wataruhusiwa kutoka nyumbani kwao kwenda kazini, hospitali na kwenda kununua mahitaji muhimu tu au kwa dharura.



Maduka yote ya bidhaa ambazo si lazima pamoja na bar na migahawa itafungwa.



Wanafunzi watasoma mtandaoni tu.



Jumla ya vifo vilivyotokea Italia siku ya Jumatatu ni 100,000 - idadi kubwa zaidi barani Ulaya baada ya Uingereza.



Maofisa wanasema maambukizi ya aina mpya ya virusi yanaongezeka .



Chanjo inafanya kazi vipi ?

Chanjo ya AstraZeneca , ambayo ilitengenezwa na Chuo Kikuu Oxford,imetengenezwa kutokana na virusi vinavyosababisha na mafua ya kawaida vilivyodhoofishwa (vinavyofahamika kama adenovirus) kutoka kwa sokwe .



Virusi hivi vimebadilishwa umbo ili kuonekana zaidi kama virusi vya corona-inagawa haviwezi kusababisha ugonjwa.



Unapochomwa chanjo hii, inaufundisha mfumo wa kinga ya mwili jinsi ya kupambana na virusi halisi, pale utakapohitaji kufanya hivyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad