Jukwaa la uchapishaji video la YouTube limeondoa video elfu 30 zenye habari za uwongo kuhusu chanjo za corona (Covid-19) zilizochapishwa tangu Oktoba 2020.
Msemaji wa kampuni ya YouTube Elena Hernandez alitoa maelezo kwa shirika la habari la The Hill na kusema kwamba video zilizoondolewa kwenye jukwaa hilo zilikuwa na madai juu ya chanjo za Covid-19 ambazo zinapingana na maafisa wa afya wa maeneo husika na Shirika la Afya Ulimwenguni.
Hernandez alisema kuwa tangu Februari 2020, YouTube imeondoa takriban video elfu 800 zenye habari za uwongo juu ya mlipuko wa janga la Covid-19.
Facebook na Twitter pia zilitoa taarifa kwamba habar za uwongo zinazochapishwa kuhusu chanjo ya Covid-19 zitaondolewa.