Mwanaharakati Edwin Kiama anayedaiwa kutengeza bango lenye picha ya Rais Uhuru Kenyatta nchini Kenya ili kulalamikia hatua ya serikali kuuchukua mkopo mwingine wa shilingi dola bilioni 255 au dola bilioni 2.34 amekamatwa na polisi.
Wanaharakati wenzake wametumia mtandao wa twitter kuitaka polisi imuachie huru baada ya kushtumiwa kwa kutekeleza uhalifu wa mtandaoni
Kiama katika bango lake alidai kwamba fedha mbazo serikali hukopa hufujwa na maafisa wakubwa .
Tangu wiki iliyopita,Wakenya wamekuwa wakilalamika mitandaoni na hata kwenye kurasa za mitandao za shirika la Fedha duniani IMF ambalo liliidhinisha mkopo huo kwa serikali.
Waziri wa Fedha Ukur Yatani hata hivyo ametetea mkopo huo mpya akisena unalenga kuisaidia Kenya kukabiliana na athari za janga la Corona na kusawazisha mzigo wa madeni ambayo Kenya inadaiwa.
Hadi kufikia sasa Wakenya wapatao 200,000 wamesaini nyaraka mitandaoni kuitaka IMF kutoipa Kenya mkopo wowote.