1: MNYAMA 🦁 ON TOP OF THE TABLE🙌 Kibabe. Kikatili Simba wameondoka na Pointi 3 ngumu ndani ya pitch kigumu kule Misungwi. MO aanze kuagiza masweta sasa.. Kileleni baridi 😀
2: Asante kocha wa Gwambina, Mohammed Badru👏 Asante Didier Gomes.. 👍 Licha ya changamoto ya pitch, makocha wametupa mechi nzuri kwenye mbinu. Kasi, nguvu na maarifa yalitawala kwa Dakika 90🙌
3: Gwambina walikuja na system ya 4-2-3-1, Kati wakianza na Holding wawili. Baraka Mtui na Kagoma walikuwa na utulivu na kasi ya kupokonya mpira huku Viungo watatu wa juu, Meshack, Jimmson na Rajab wakiwa wakiwapress vyema mabeki wa Simba ili kuwanyima nafasi ya kuanza shambulizi kwa kupiga 'Long Balls'
4: Didier Gomes aliswitch kutoka kwenye 4-2-3-1 na kuja na 4-1-3-2 akiwa na Plan ya kucheza kwa mipira mirefu, akiutoa mpira katikati ya kiwanja kukwepa changamoto ya pitch
5: Always.. Mechi ngumu kwenye mbinu huamuliwa na 'quality' za wachezaji kuamua mchezo. Hapa ndipo tofauti ilipokuja.. Quality ya Simba ikaidhibu Gwambina. Kivipi?
6: Rudi na ulitazame tena na tena bao la MOHAMMED HUSSEIN🙌 Moderm Football it's all about Space and Time. Ile First touch ya Tshabalala ni ya Thamani sana. Ndani ya sekunde chache mpira ukiwa angani, brain yake ikafikiri kwa haraka na kuamua.. WHAT A GOAL🙌
7: Gwambina imepoteza lakini Yule kipa wao Mohammed Makaka alikuwa kwenye kiwango bora sana 👍 Simba walicheza kwa malengo na Attempt zao zilikuwa ON TARGET.. Mikono ya Makaka ilikuwa kwenye ubora sana.
8: Onyango🙌 INATOSHA SASA KUMUELEZEA. Kile ni KITASA cha Guantanamo 🙌 Anacheza kwenye kila mdundo wa mpinzani. Ukiweka Reggea, mnaruka nae. Ukiweka singeli, mnalimwaga nae.. What A Player🙌
9: Lile tukio la Onyango linabaki kwenye maamuzi ya Line 1. Katika mstari aliosimama, yeye ndio mwenye nafasi ya kuona vyema muelekeo wa ule mpira ukiwa angani
10: Welld done Jimmson Mwanuke💪 Mchezaji mkubwa kwenye jezi ya timu ndogo. Anajua sana. WELL PLAY GUSTAVO. Na udogo wake vilevile, Alimstopisha Kisinda na leo kammeza Morrison..
Nb: Kwani Wananchi wenyewe Wanasemaje 😀