Aliyekuwa gavana Nairobi akutwa na corona licha ya kupata chanjo




Aliyekuwa Gavana wa Jimbo la Nairobi nchini Kenya, Evans Kidero, amekutwa na virusi vya Corona, wiki moja tangu achomwe sindano ya chanjo ya ugonjwa wa COVID-19.

Facebook: Evans Kidero

Kidero amesema alipatikana na ugonjwa huo Jumanne, Aprili 6, wakati ambao yeye na familia yake walipokwenda kufanya vipimo baada ya kuonesha dalili za corona.

Kwa mujibu wa Gavana huyo wa zamani, amesema alikutwa na virusi hivyo vya corona wiki moja baada ya kupatiwa chanjo ya ugonjwa huo mnamo Machi 29, 2021.

Aliongeza kusema wengine katika familia yake walipimwa lakini hawakukutwa na Corona.

Sasa Kidero atakuwa akijitenga kwa muda wa wiki mbili zijazo.

Taarifa hii inakuja wakati serikali ya Kenya ikianza kufanya uchunguzi wa madai kwamba mgonjwa mmoja alifariki baada ya kuchomwa sindano ya chanjo dhidi ya Covid-19.

Mapema leo katika mkutano na wanahabari, Dkt. Peter Mbwiiri Ikamati, Naibu Mkurugenzi wa Bodi ya Dawa na Sumu nchini kenya, amesema kwamba walikuwa wakichunguza kifo kilichotokea kwa raia mmoja wa Kenya kupokea chanjo na kufariki, na kuongeza kuwa jumla ya watu 279 wameathiriwa vibaya baada ya kupokea chanjo hiyo.

Lakini muda mfupi baadae, Dkt. Collins Taabu – mkuu wa Programu ya Chanjo ya Kitaifa – alikanusha hilo, akisema hakuna uhusiano na kwamba bado haijafahamika ikiwa kifo hicho kilisababishwa na chanjo hiyo.

“Bora tu umepewa chanjo, chochote kitakachokupata baadae kitaangaliwa, kuchunguzwa, na kuripotiwa. Ndio maana tunafuatilia kesi hii, ”alisema Dkt. Ikamati.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad