Baraza la Ulamaa lateua masheikh 19 wa mikoa





Baraza  Kuu la Ulamaa la Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata) chini ya mwenyekiti wake, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir limefanya uteuzi wa masheikh wa mikoa 19.


Wajumbe wa baraza hilo walikaa jana  Aprili 4, 2021 na kufanya uteuzi huo kwa mujibu wa katiba ya Bakwata.



Uteuzi wa masheikh hao wa mikoa umetangazwa leo Jumatatu Aprili 5, 2021 na msemaji wa Mufti, Khamis Mataka.



Mataka aliwataja miongoni mwa masheikh wa mikoa walioteuliwa ni pamoja na Alhad Mussa Salum ( Dar es Salaam), Shaaban Juma (Arusha), Mustafa Rajab ( Dodoma) na  Mohammad  Mushangani wa Lindi.



Katika hatua nyingine, Sheikh Mataka amesema Mufti Zubeir amewateua wajumbe tisa wa baraza la Ulamaa ambao ni pamoja na Sheikh Hamid Jongo, Ally Khamis, Shaaban Msuya, Issa Othman  na Mkowe Abdallah.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad