Billnass amefunguka kusema anashangaa watu wanaosambaza taarifa kwamba ameachana na mpenzi wake Nandy kwa sababu hajawahi kuongea lolote kuhusu hali yake ya mahusiano kwa sasa.
Billnass amesema watu wanakosea kusambaza taarifa hizo na wala hazihusiani na kile alichokiimba kwenye wimbo wake mpya wa tatizo ambapo mashabiki wengi wametafsiri kama amemchana Nandy.
"Mimi sijawahi kuzungumza popote kuhusu suala langu la mahusiano na hakuna mtu ambaye nimetaka aone kwamba nieleze ishu ipo hivi au vile, nimeamua kufanya kazi yangu ila tatizo kubwa ni kuanza na ukurasa mpya, watu wanakosea" amesema Billnass