Kasri ya Buckingham imesema mume wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, Prince Philip amefariki dunia leo Ijumaa, Aprili 9, 2021, akiwa na umri wa miaka 99 katika Kasiri la Windsor. Takribani miezi miwili iliyopita, Februari 16 aliugua na kulazwa katika Hospitali ya King Edward VII, London ambapo Machi 16 aliruhusiwa na kurejea kwenye Kasiri. Bado haijaelezwa amefariki kwa ugonjwa gani.
Prince Philip alimuoa Princess Elizabeth mwaka 1947, miaka mitano kabla ya kusimikwa kuwa Malkia wa Taifa hilo, na amekuwa msaidizi mzuri zaidi wa malkia kwenye historia ya Uingereza.
Kwa mujibu wa taarifa ilitolewa na ikulu ya Malkia Buckingham, imesema Malkia amesikitishwa na kifo cha mumuwe mpendwa Prince Philip, ambacho kimeacha huzuni kubwa kwa familia yake.
Malkia Elizabeth na Prince Philip wamejaliwa kupata watoto 4, wajukuu 8, na vitukuu 10.
“Ni kwa masikitiko makubwa, Malkia ametangaza kifo cha mumewe mpenzi, Mwanamfalme Philip, Duke (Mtawala) wa Edinburgh. Mwanamfalme Philip amefariki kwa amani asubuhi ya leo katika Kasri la Windsor.” Mwanamfalme Philip “alipata mapenzi ya vizazi” – Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.
Boris anasema ni “kwa huzuni kubwa” kupokea habari za kifo cha Mwanamfalme Philip kutoka Kasri la Buckingham. Akitoa salamu zake za rambirambi alisema Mwanamfalme Philip alipata mapenzi ya vizazi nchini Uingereza, katika Jumuiya ya Madola na ulimwenguni kote.
“Alikuwa mshirika wa kifalme aliyehudumu kwa muda mrefu katika historia, mmoja wa watu wa mwisho nchi hii kuwahi kutumika katika Vita vya pili vya na alitajwa katika barua za ushujaa.”
Katika rambirambi zake, Boris Johnson alisema, “alisaidia kuongoza familia ya kifalme na ufalme ili iweze kuwa taasisi muhimu bila shaka kwa usawa na furaha ya maisha yetu ya kitaifa.”
Boris Johnson anamaliza rambi rambi zake kwa kusema kwamba Familia ya Kifalme wamepoteza “sio tu mtu anayependwa sana na anayeheshimiwa sana na umma, lakini mume aliyejitolea, baba mwenye fahari na mwenye upendo, babu, na katika miaka ya hivi karibuni, babu-mkubwa”.
Waziri mkuu anamnukuu Malkia wakati mmoja akisema nchi hiyo inadaiwa na mumewe deni kubwa kuliko “tunavyopaswa kujua”, na kuongeza kuwa alikuwa na hakika kuwa makadirio hayo yalikuwa sahihi.
‘Tunaomboleza leo na Malkia, tunampa pole zetu, na familia yake yote na tunashukuru, kama taifa, na ufalme, kwa maisha ya kipekee na kazi ya Mwamfalme Philip, Mtawala wa Edinburgh,” alisema.
Mwanamfalme Philip alimuoa Bintimfalme Elizabeth mnamo 1947, miaka mitano kabla ya kuwa Malkia, na amekuwa mwenza wa mfalme ama malkia aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.
Walikuwa na watoto wanne ,wajukuu wanane na vitukuu 10. Mtoto wao wa kwanza, Mwanamfalme Charles, alizaliwa mwaka 1948, akifuatiwa na dada yake, Bintimfalme Anne mwaka 1950. Mtoto wao wa tatu Mwanamfalme Andrew alizaliwa mwaka 1960 na mtoto wao wa mwisho Mwanamfalme Edward alizaliwa mwaka 1964.
Mwanamfalme Philip alizaliwa katika kisiwa cha Corfu nchini Ugiriki Juni 10, 1921. Baba yake alikuwa Mwanamfalme Andrew wa Ugiriki na Denmark, ambaye alikuwa ni mtoto wa mwisho wa kiume wa Mfalme George I wa Hellenes. Mama yake, Bintimfalme Alice, alikuwa ni mtoto wa Bwana Louis Mountbatten na kitukuu cha Malkia Victoria.
L