Jose Mourinho aliyekuwa Kocha Mkuu wa Tottenham Spurs amefutwa kazi rasmi leo Aprili 19.
Kocha huyo alijiunga na Spurs akichukua mikoba ya Mauricio Pochentino ambaye kwa sasa anaifundisha Klabu ya PSG.
Baada ya kuibuka ndani ya Spurs alianza kwa kasi nzuri ila ghafla mambo yakawa magumu kwake kwa timu hiyo kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zake za Ligi Kuu England pamoja na mechi nyingine za ushindani.