Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza kuwa kituo cha televisheni cha Clouds kililipwa Sh 629.7milioni na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kiasi cha Sh201.4 milioni kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya tamasha la urithi lakini hakukuwa na risiti zozote za kielektroniki zilizotolewa kuthibitisha malipo hayo.
Akizungumza leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema kodi ya zuio ya Sh31 milioni na Sh10 milioni kutoka Clouds na TBC hazikukatwa kutoka katika malipo hayo.
“Wizara haikutimiza wajibu wake katika kukata hiyo kodi ya zuio, vilevile sikupewa ushahidi ukionyesha kuwa manunuzi ya huduma za matangazo kutoka TBC na Clouds yalipatikana kwa ushindani ulio sawa,”