Chad: Mwanae Idris Deby achukua uongozi wa nchi baada ya kifo cha baba yake






Mwanae Idris Deby amechukua usukani wa Chad huku waasi wakiapa kuimarisha mashambulizi ya pamoja.
Kifo cha ghafla cha Rais wa Chad Idriss Deby kimemfanya mwanae , Luteni Mahamat Idris Deby Itno (al maaruafu General Kaka), kuwa uongozi wa taifa hilo la Afrika ya kati, kwa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja kabla kufanya uchaguzi.

Waasi wanatishia kufanya upya mashambulizi dhidi ya mji mkuu N’Djamena.

Mahamat, mwenye umri wa miaka 37, jana alitangaza Baraza la Mpito la wanajeshi la wanachama 15 (TMC) linaloundwa na majenerali ambao wataiawala Chad kwa miezi 18 ijayo.

Baraza la mawaziri na Bunge lilivunjwa na amri ya kitaifa ya kutotoka nje imewekwa.Waasi kutoka chama cha Front for Change and Concord in Chad (FACT) wameripotiwa kuanza tena harakati zao kuelekea N'Djamena, baada ya kifo cha Deby.

Deby, ambaye aliongoza Chad kwa miongo mitatu, alifariki saa kadhaa baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Aprili 11 na karibu 80% ya kura.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii jana usiku, FACT ilisema: "Vikosi vya upinzaji viko katika milango ya N'Djamena.

''Tuko hapa kupiga kengele, sio za chuki au mgawanyiko, bali kupiga kengele za amani na matumaini mapya. Na zitakapolia, hakutakuwa na mikono tena nchini Chad kupiga ngoma za vita. " ilisema taarifa hiyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad