Cosota Yatoa Somo La Hakimiliki Kwa Maprodyuza Wa Muziki




Anitha Jonas – COSOTA
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki, Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare atoa elimu kwa Watayarisha wa Muziki nchini (Maprodyuza) kwa kuwaeleza umuhimu wa kusimamia haki zao na  kuingia mikataba na wasanii pale wanapokuwa wanafanya kazi zao.

Mtendaji huyo  ametoa elimu hiyo katika kikao cha Uzinduzi wa Chama cha Umoja wa Maprodyuza Tanzania (Tanzania Producers and Composers Association) kilichofanyika Aprili 17, 2021 Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanya uchaguzi  wa viongozi pamoja na kuweka mikakati ya namna ya kuendesha chama hicho ambacho kimeanzishwa hivi karibuni.

"Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inaweka  ulinzi katika kazi za Sanaa na usimamizi madhubuti  wa Hakimiliki na serikali inataka sekta ya Sanaa ikue na kuendana na kipato na siyo mtu anakuwa na umaarufu wa jina halafu kipato chake kinakuwa hakiendani na umaarufu wake "alisema Bibi Doreen.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo wa TPCA  Bibi. Doreen alieleza kuhusu Mfuko wa Sanaa na Utamaduni ambao  unatarajia kuzinduliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na pale utakapozinduliwa utawanufaisha wadau wote wa sekta ya Sanaa na Utamaduni kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu, pamoja na kusaidia kutoa ufadhili wa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika kuimarisha ujuzi katika kazi zao.

Kwa upande wa Muanzilishi wa Chama hicho Prodyuza P-Funk Majani alitoa ombi kwa COSOTA  la kusambaza sampuli za Mikataba  na fomu za Usajili na kutaka Studio zote nyaraka hizo ili mteja anapokwenda kuandaliwa kazi ahakikishe anasaini mkataba na studio pamoja na kujaza fomu ya COSOTA studio, ili ulinzi wa kazi kuanza katika ngazi ya chini.

Aidha, nae mmoja wa Maprodyuza hao Quick Raca atoa maoni kuwa ya kuiomba COSOTA kuwa na mfumo wa kusimamia matumizi ya kazi za wanamuziki kwa kutoa msisisitizo  kwa Makampuni  yaliyosaini mikataba na wasanii peke yao kwa kazi zinazohusisha haki za "Maproducer"  makampuni hayo sasa yaingie mikataba pia na ‘Producers’ ili yaanze kulipa na "producers", na kuanzia sasa  utaratibu wote upitie COSOTA vilevile  matumizi ya kazi za muziki kwenye mitandao yote ilipwe na wanaotumia, halikadhalika Televisheni na Redio zisipige au kuonyesha kazi ya Muziki kama haijapita kukaguliwa BASATA, Bodi ya Filamu Tanzania na kusajiliwa COSOTA.

Pamoja na hayo Maprodyuza hao waliridhia ushauri wa kuanza  kujisajili kwenye chama chao na pia kujisajili COSOTA na kusajili kazi zao COSOTA na  kwa taasisi zinazowasimamia pamoja na kuanza kuwa na utaratibu wa kutumia mikataba katika kazi zao.

Halikadhalika  Doreen  aliahidi  kuwa COSOTA itatoa  sampuli ya mikataba   hiyo bure na zitakabidhiwa TPCA ili kuweza kuwafikishia wadau hao. Pia aliwasisitiza kuwa umoja wao ukiwa imara na wenye manufaa wadau wengi wanaweza kujiunga na kunufaika zaidi.hivyo ni vyema wajenge misingi imara ya kukuza tasnia hiyo kwa lengo la kuweza kunufaika vyema na kazi zao. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad